
------------------------------------------
Mara Online News
--------------------------
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Agnes Meena, leo Novemba 16, 2023 amezindua Maonesho ya Nane ya Kilimo Mseto yanayofanyika kwenye viwanja vya ATC, Bweri mjini Musoma, Mara.
Maonesho hayo ya siku tatu [Novemba 16 – 18, 2023], yameandaliwa na VI Agroforestry, na yanafanyika sambamba na Maadhimisho ya Miaka 40 ya shirika hilo.


Naibu Katibu Mkuu Dkt Agnes pia amepata fursa ya kupita na kukagua bidhaa kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho hayo - yenye kaulimbiu inayosema: “Panapostawi Miti - Watu Hustawi”.
No comments:
Post a Comment