NEWS

Tuesday 21 November 2023

Shule tatu Nyamongo zapokea misaada kutoka Kampuni ya KemanyankiMeneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Kemanyanki, Selina Mkaro akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamongo msaada wa fedha taslimu, leo Novemba 21, 2023.
---------------------------------------------------

Na Mwandishi wa Mara
Online News, Nyamongo
-----------------------------------


SHULE tatu zilizopo Nyamongo - jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, zimepokea misaada ya shilingi milioni 5.6, mipira na jezi za michezo kutoka Kampuni ya Kemanyanki.

Shule ya Msingi Nyamongo imepewa mipira miwili, jezi za michezo na fedha taslimu shilingi milioni 1.5, kwa ajili ya kuwalipa walimu wanaojitolea kufundisha shuleni hapo.


Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Kemanyanki, Selina Mkaro na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamongo, baada ya kuwakabidhi msaada wa mipira na jezi za michezo.
Nyingine ni Shule ya Sekondari Nyamongo ambayo imepewa shilingi milioni 3.6, kwa ajili ya kulipa pia mishahara ya mwalimu wa Fizikia wa kujitolea kwa mwaka mzima wa 2024.

Nayo Shule ya Sekondari Ingwe imepewa msaada wa shilingi 500,000 kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi wa TYSCS.


Selina (kulia) akimkabidhi mmoja wa viongozi wa TYSCS Shule ya Sekondari Ingwe msaada wa fedha.
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Kemanyanki, Celina Mkaro amekabidhi misaada hiyo kwa viongozi wa shule hizo, leo Novemba 21, 2023.

Selina amesema wametoa misaada hiyo baada ya kuombwa na viongozi wa shule hizo kwa nyakati tofauti, na kwamba wanafanya hivyo kurudisha sehemu ya faida yao kwa jamii inayozunguka mgodi wa North Mara.


Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyamongo (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Kemanyanki.
Kemanyanki ni moja ya kampuni za wazawa ambazo zinatoa huduma mbalimbali katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, unaoendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania, kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Wananchi wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara pia wana kila sababu ya kujivunia uwepo wa Kampuni ya Kemanyanki na mgodi huo kutokana na kuwatengenezea fursa za ajira na biashara za kuwakwamua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages