NEWS

Wednesday 22 November 2023

UWT Wilaya ya Serengeti wamtunuku Chandi tuzo maalum kutambua mchango wake ndani ya CCMMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (kushoto) na Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Serengeti, Morobanda Japan wakionesha tuzo maalum ambayo kiongozi huyo wa mkoa ametunukiwa na UWT Wilaya ya Serengeti leo Jumatano. Kulia ni Katibu wa UWT Serengeti, Mary Kananda.
----------------------------------------------------

Na Mwandishi wa Mara
Online News, Serengeti
---------------------------------


Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Serengeti umemtunuku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi tuzo maalum ya kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa katika kukijenga na kukiimarisha chama hicho tawala wilayani na mkoa huo kwa ujumla.

Chandi amekabidhiwa tuzo hiyo na Katibu wa UWT CCM Wilaya ya Serengeti, Mary Kananda, kabla ya kiongozi huyo wa mkoa kuhutubia kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya na mikutano mingine ya wananchi leo Novemba 22, 2023.


UWT Serengeti wakiendelea kumpngeza Mwenyekiti Chandi kwa zawadi nyingine mbalimbali.
Mwenyekiti Chandi amewasili na kupokewa na viongozi wa chama hicho wilayani Serengeti leo kuendelea na ziara yake ya kuimarisha chama hicho tawala, kukagua maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.

Mapokezi ya Chandi yameongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Serengeti, Morobanda Japan, ambapo kiongozi huyo wa mkoa alikagua na kushiriki kwa vitendo ujenzi wa jengo la nyumba ya makazi ya Katibu wa CCM Wilaya.

Kisha Mwenyekiti Chandi amepata fursa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya tawi la MCU, kabla ya kutembelea jengo la kitega uchumi cha CCM lililopo mjini Mugumu.
Chandi akisindikizwa na viongozi wengine kukagua jengo la kitega uchumi cha CCM lililopo mjini Mugumu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages