NEWS

Friday 22 December 2023

Kamati ya Usalama Barabarani Tarime Rorya yafanya ukaguzi wa kushtukiza kwa madereva na magari ya abiria




Na Mwandishi wa
Mara Online News
------------------------------


KAMATI ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, mapema leo asubuhi, Ijumaa Disemba 22, 2023 imefaya ukaguzi wa kushtukiza kwa madereva na magari ya abiria katika stendi ya Tarime Mjini.

Ukaguzi huo umehusisha kupima ulevi kwa madereva na ufungaji mikanda kwa abiria.

Aidha, wajumbe wa kamati hiyo wametumia nafasi hiyo pia kuelimisha abiria umuhimu wa kufunga mikanda wanapokuwa safarini.

Pia wameelimisha madereva umuhimu wa kuzingatia na kufuata sheria za usalama barabarani, lakini pia kuepuka kuendesha magari kwa mwendo kasi.



Ukaguzi na uelimishaji huo umeongozwa na Mwenyekii wa Kamati hiyo, Ernest Oyoo na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa (RTO) wa Tarime wa Rorya, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Mbunja Matibu.

Kwa mujibu wa viongozi hao, lengo la ukaguzi huo ni kuhakikiksha usalama wa magari na abiria unazingatiwa, hususan kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages