NEWS

Tuesday 19 December 2023

Rais Samia amteua Dkt Nyansaho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCODkt Rhimo Simeon Nyansaho
-----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
------------------------------


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ameivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) na kumteua Dkt Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo.

Dkt Nyansaho ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania, na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo - ambaye Desemba 18, 2023 aliteuliwa na Rais Samia kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus jijini Dar es Salaam jana, ilisema uteuzi huo wa Dkt Nyansaho unaanza mara moja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages