NEWS

Monday 4 December 2023

Sabaya aliyewahi kuwa DC Serengeti sasa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Arusha


Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy Thomas Sabaya.
-------------------------------------------
Na Mwandishi
Wetu, Arusha
----------------------


Aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya (DC) ya Serengeti, Loy Thomas Sabaya ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, katika uchaguzi maalum ulifanyika leo Jumatatu.

Taarifa za hivi bunde kutoka ukumbi wa IACC Arusha zinasema Sabaya ametangzwa mshindi baada ya kuvuna kura 463 kati ya 907 zilizopigwa katika kinyang’anyiro hicho.

Katika mchuano huo, Sabaya amewabwaga wagombea wenzake ambao ni Dkt Daniel Mrisho Pallangyo aliyepata kura 374, Solomoni Olesendeka Kivuyo (59) na Edna Israel Kivuyo aliyeambulia kura 10.

Sabaya anatajwa kuwa pamoja na mambo mengine, akiwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti katika Serikali ya Awamu ya Tatu alifanya kazi kubwa kukomesha wizi wa mifugo, ujangili na kuhamasiha shughuli za maendeleo, ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari.

Uchaguzi huo umefanyika kuziba pengo lililoachwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Zelothe Stephen aliyefariki dunia Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages