NEWS

Monday 4 December 2023

Barrick yang'ara tuzo 5 kutoka Chama cha Waajiri Tanzania
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
-------------------------------------------------


Kampuni ya Barrick Tanzania ina kila sababu ya kujivunia ubora, baada ya jana kushinda tuzo tano za Mwaka wa Tuzo zilizotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Tuzo ya kwanza katika kundi la Mwajiri Bora kwa Uwajibikaji kwa Umma ilikwenda kwenye kampuni maarufu ya Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ulioko Tarime, mkoani Mara.

Zawadi ya pili ya kundi la Ubora wa Menejimenti Wakati wa Migogoro ilinyakuliwa na Mgodi wa Bulyanhulu uliopo katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Hali kadhalika, zawadi ya Mshindi wa pili katika kundi la ‘Local content’ ilichikuliwa na Mgodi wa North Mara, ambao pia ulijizolea zawadi katika makundi ya Mwajiri wa Shirika Kubwa Bora la Mwaka 2023 na Mshindi Bora wa Jumla katika Sekta Binafsi.

Migodi hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serekali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages