NEWS

Tuesday 12 December 2023

Wakulima Tarime Vijijini walilia kiwanda cha kusindika ndizi



Mratibu wa MVIWANYA, Joel Nguvava (mwenye fulana ya bluu) akigawa mbegu za maharage aina ya Funika kwa wakulima katika kijiji cha Nyarero wilayani Tarime, jana Jumatatu.
----------------------------------------------------

Na Mwandishi wa Mara
Online News, Tarime
---------------------------------


SERIKALI imeombwa kujenga kiwanda cha kusindika ndizi katika wilaya ya Tarime mkoani Mara, ili kuliongezea thamani zao hilo, na kuwezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.

Ombi hilo lilitolewa na wakulima wa ndizi katika kata za Nyarero na Muriba, wakati wa mafunzo ya kuongeza mnyororo wa thamani kwenye zao la ndizi, yaliyofanyika kwa nyakati tofauti katika kata hizo jana Jumatatu, chini ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima na Wafugaji Nyancha (MVIWANYA).

Mkulima na mwanachama wa kikundi cha Reng'anya kijijini Nyarero, Samson Muginga, alisema kiwanda cha kusindika ndizi kitawaondolea wakulima kero ya kunyonywa na madalali wa biashara ya zao hilo.


Samson akifafanua jambo.

“Tunaomba tujengewe kiwanda cha kuchakata zao la ndizi hapa Tarime maana kutokuwepo kwa kiwanda hicho kunasababisha kwa mfano mkungu wenye thamani ya shilingi elfu kumi kununuliwa chini ya elfu tano,” alisema Muginga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kikundi cha Rekong'ai, Selina Nyangi, alitaja mahitaji mengine ya wakulima wa wilayani Tarime kuwa ni pamoja na mafunzo endelevu ya kilimo mesto, na masoko ya uhakika.


Selina akizungumza.

“Elimu ya kilimo mseto iwe endelevu na soko la uhakika ili akina mama na vijana tupige hatua na Taifa lipate maendeleo,” alisema Nyangi.

Mbali na kuwezesha mafunzo hayo, Mratibu wa MVIWANYA, Joel Nguvava aliwagawia wakulima hao mbegu za maharage aina Funika isiyohitaji mbolea na ambayo inahimili hali za ukame na mvua.


Nguvava akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.

MVIWANYA hutekeleza shughuli zake chini ya ufadhili wa Shirika la Vi Agroforestry ambalo limejikita katika kuwezesha wakulima kufundishwa mbinu bora za kilimo endelevu - kisicholeta athari za kimazingira.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages