Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa, Moses Jacob (kushoto) akikabidhi msaada wa shilingi 200,000 kwa Kamati ya Ujenzi wa Zahanati ya Kebosongo zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Mara, Patrick Chandi kuchangia gharama za fundi wa ujenzi wa zahanati hiyo jana.
--------------------------------------------------
Mara Online News
--------------------------
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi, ametoa shilingi 200,000 kuchangia gharama za fundi wa ujenzi wa Zahanati ya Kebosongo iliyopo kata ya Kisangura wilayani Serengeti.
Msaidizi wa Mwenyekiti Chandi, Moses Jacob ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mara, alikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa uongozi wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo jana.
“Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Chandi amenituma niwaletee kiasi hiki cha fedha kama ambavyo mlimwomba kwamba mmepungukiwa sehemu, akaahidi kuwa atawachangia ili kukidhi mahitaji,” alisema Jacob.
Wajumbe na viongozi wa Kamati ya Ujenzi wa Zahanati ya Kebosongo, akiwemo Diwani wa Kata ya Kisangura, Samson Ryoba Wambura (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja mbele jengo la zahanati hiyo jana.
----------------------------------------------
Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa kata ya Kisangura, Diwani Samson ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, alimshukru Chandi kwa moyo wake wa kujitolea kwa hali na mali kutumikia na kusaidia wananchi mkoa wa Mara.
Diwani huyo alitumia nafasi hiyo pia kumwomba Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Mara kutochoka kuwasaidia wananchi hao ili waweze kufungua zahanati hiyo mapema mwaka huu.
“Kwa sasa tuko hatua nzuri ya usajili wa zahanati, kuleta umeme, jengo la mama na mtoto limeishakamilika ila bado ‘finishing’ ndogo ndogo,” alisema.
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mara, Jacob, hivi karibuni alikabidhi shilingi 100,000 kwa niaba ya Mwenyekiti Chandi - kuchangia gharama za ununuzi wa samani za ofisi ya watu wenye ulemavu katika kata ya Kibara wilayani Bunda.
No comments:
Post a Comment