NEWS

Tuesday 13 February 2024

Naibu Katibu Mkuu Mwajuma ahimiza wadau kuongeza nguvu ya kutafuta fedha za majiNaibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri.
---------------------------------------

Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
-----------------------------


NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri amewataka wadau wa sekta mtambuka kuongeza nguvu zaidi za kupata fedha na kushirikiana na Serikali katika kufanikisha masuala anuai yahusuyo huduma ya maji kwa Watanzania.

Mhandisi Mwajuma amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akifunga Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji.

Amesisitiza umuhimu wa kuongeza wadau wa Jukwaa hilo ili kuyafikia makundi mengi katika jamii, lakini pia kuongeza nguvu ya ushirikishwaji.

Amesema ni muhimu kuwa na mipango inayotekelezeka ya kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyokubalika kwa jamii.

Mhandisi Mwajuma ni mmoja kati ya vinara wanawake katika masuala ya uhandisi na huduma kwa jamii hapa nchini.

Mkutano huo umefanyika kwa siku mbili ukiwa umebeba kaulimbiu isemayo: “Majanga ya Mafuriko na Ukame: Uwekezaji katika Usalama wa Maji ni Jambo la Haraka.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages