NEWS

Monday 5 February 2024

Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji: Wizara husika yatoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa, wilaya



Waziri Dkt Dorothy Gwajima
----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
-----------------------------------------


KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji hapo kesho Jumanne, Serikali imetoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanawashirikisha wadau na viongozi wote wa kijamii, na kuwezesha maadhimisho hayo kufanyika katika ngazi zote.

Akitoa maelekezo hayo jijini Dodoma hivi karibuni, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima alielekeza maadhimisho hayo yafanyike katika ngazi zote, yakijumuisha kutembelea shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuwajengea watoto uwezo wa kupinga ukeketaji, kuendesha midahalo na kutoa elimu kuhusu madhara ya vitendo hivyo.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria (TDHS-2022), kiwango cha ukeketaji nchini Tanzania kimepungua na kupanda katika sehemu mbalimbali, huku mikoa ya Mara, Singida, Manyara, Dodoma na Arusha ikionekana kuongoza kwa ukatili huo wa kijinsia.

Maadhimisho hayo yanayolenga kutokomeza ukeketaji kwa wanawake na watoto, ambapo kaulimbiu yake mwaka huu inasema: “Sauti yangu, Hatima yangu, Wekeza kwa Manusura Kutokomeza Ukeketaji”.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages