NEWS

Tuesday 27 February 2024

Waziri Mkuu aiagiza Wizara ya Madini kuratibu majadiliano ya fidia mgodi wa North Mara na wananchi



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 
akizungumza na wananchi jana.
------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Mara
------------------------------------


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Madini kuratibu majadiliano ya suala la fidia kati Mgodi wa Dhahabu wa North Mara na wananchi wanaouzunguka ili kuwepo na maridhiano ya pamoja.

Majaliwa alitoa maelekezo hayo jana Jumanne wakati akizunguumza na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) eneo la Nyamwaga, kilomita chache kutoka mgodini hapo.

Aliekeleza kuwepo na kikao maalum kitakachoshirikisha wananchi na uongozi wa mgodi huo ili kupata mwafaka mzuri.

“Wajipange waje siku maalum wawe na kikao cha pamoja na wananchi na mgodi ili kuwe na maridhiano yatakayofika mwisho. Suala la kila kiongozi wa kitaifa akipita hapa [Nyamongo] fidia, fidia nalo liishe,” alisisitiza Majaliwa ambaye yupo katika ziara ya kikazi ya siku tano mkoani Mara.

Mtendaji Mkuu huyo wa Serikali alisisitiza kuwa suala hilo haliwezi kuchukuliwa kwa wepesi, lazima lifike mwisho.

Mgodi wa North Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick Gold kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kamapuni ya Twiga Minerals.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages