NEWS

Wednesday 28 February 2024

Chandi amwomba Waziri Mkuu uwanja wa ndege, soko la kisasa MugumuWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa 
akiwa wilayani Serengeti jana.
--------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Serengeti
---------------------------------------


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi amewasilisha kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa maombi ya ujenzi wa uwanja wa ndege, barabara za lami na soko la kisasa katika mji wa Mugumu.

Chandi aliwasilisha maombi hayo wakati Waziri Mkuu Majaliwa alipowasili wilayani Serengeti jana Jumanne kuendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

Mwenyekiti Chandi
--------------------------

Mwenyekiti huyo wa chama tawala alisema ujenzi wa miundombinu hiyo utachochea shughuli za kitalii, miongoni mwa maendeleo mengine ya kiuchumi na kijamii katika wilaya hiyo ambayo eneo lake kubwa ni Hifadhi ya Taifa Serengeti.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages