NEWS

Wednesday 27 March 2024

Jumuiya ya Mt Laurent kutoka Parokia ya Tarime yapeleka msaada Mji wa Huruma Kigera Tuma- MusomaBaadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Mt Laurent kutoka Kanisa Katoliki la Yosefu Mfanyakazi, Parokia ya Tarime wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wagonjwa wanaotunzwa katika Mji wa Huruma Kigera Tuma.
----------------------------------------------

NA MWANDISHI WETU, Musoma
----------------------------------------------


JUMUIYA ya Mt Laurent kutoka Kanisa Katoliki la Yosefu Mfanyakazi, Parokia ya Tarime, imetembelea kituo cha Mji wa Huruma Kigera Tuma kilichopo Musoma mkoani Mara, na kukabidhi msaada wa vyakula mbalimbali na fedha taslimu kwa ajili ya mahitaji ya wagonjwa wa akili wanaotunzwa kituoni hapo.

Msaada huo ulitokana na michango ya hiari iliyotolewa na wanachama wa Jumuiya hiyo kuonesha upendo, huruma majitoleo yao kwa wagonjwa hao.

Ziara ya kupeleka msaada huo ilifanyika Jumamosi iliyopita, ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mwl Johnbosco Nyitambe na Mweka Hazina, Mwl Laurent Mwita.

Aidha, wanachama wa Jumuiya hiyo walipata fursa ya kushiriki ibada fupi pamoja na baadhi ya wagonjwa wanaotunzwa katika kituo hicho cha Mji wa Huruma Kigera Tuma, kabla ya kukaribishwa kula nao chakula cha mchana.

Mama wa Nyumba wa kituo hicho, Salome Achllaus aliishukuru Jumuiya hiyo ya Mt Laurent kwa moyo wa upendo iliouonesha kwa wagonjwa hao, na akaiombea baraka nyingi kwa Mwenyezi Mungu.
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages