NEWS

Thursday 28 March 2024

Viongozi, wananchi wafika nyumbani kwa MNEC Gachuma mjini Tarime kumpa pole kwa kufiwa na mke wakeMkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima (kushoto), Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Said Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), na viongozi wengine wakiwa nyumbani kwa MNEC Chiristopher Mwita Gachuma (wa pili kutoka kushoto) Bomani mjini Tarime kumpa pole kwa kufiwa na mke wake, Francisca.
---------------------------------------------

Na Mara Online News, Tarime
-----------------------------------------


VIONGOZI mbalimbali wa Chama, Serikali na Madhehebu ya Dini, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida, wamefika nyumbani kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Christopher Mwita Gachuma, kumpa pole kwa kufiwa na mke wake, Francisca.

Miongoni mwa viongozi walioshuhudiwa leo Alhamisi wakiwa nyumbani kwa MNEC Gachuma eneo la Bomani mjini Tarime, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Said Meck Sadiki na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi.


Viongozi wa CCM, Chandi na Ngicho 
msibani nyumbani kwa MNEC Gachuma.
-------------------------------------------

Wengine waliofika msibani hapo ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho, viongozi mbalimbali wa dini akiwemo Askofu Joshua Maswi wa EAGT Tarime Mjini, na mfanyabiashara maarufu, Peter Zakaria, miongoni mwa wengine.


Mwenyekiti Chandi akisaini kitabu 
cha maombolezo msibani hapo.
-----------------------------------------


Mwili wa mama Francisca unatarajiwa kuagwa rasmi nyumbani hapo kesho Ijumaa, kabla ya kusafirishwa kwenda kwa Gachuma kijijini Komaswa kwa ajili ya mazishi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages