
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko na mke wake, Bernadetha wakimpa pole MNEC Christopher Mwita Gachuma (kushoto) nyumbani kwake kijijini Komaswa, Tarime leo Machi 31, 2024 kwa kufiwa na mke wake, Francisca,
---------------------------------------------
---------------------------------------
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko amefika kijijini Komaswa katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kuhani msiba wa mke wa Christopher Mwita Gachuma, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama tawala - CCM.
Dkt Biteko akiwa ameambatana na mke wake, Bernadetha wamefika msibani hapo leo Machi 31, 2024, ikiwa ni siku moja baada ya mke wa Gachuma, Francisca (74) kuzikwa nyumbani kwake kijijini Komaswa.
Hafla ya mazishi ya Francisca ambaye pia alikuwa Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community (NLGCC) Jimbo la Mara Kaskazini, ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment