NEWS

Monday 25 March 2024

Prof Muhongo hakamatiki Musoma Vijijini, aendelea kugawa vitabu vya utekelezaji Ilani, simu za kusajii wana-CCMMbunge wa Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo (mwenye fulana nyeusi) akiwa na baadhi ya viongozi katika kata ya Suguti, wakionesha vitabu vya utekelezaji wa Ilani ya CCM walivyogawiwa wiki iliyopita.
------------------------------------------------

NA MWANDISHI WETU, Musoma
-------------------------------------------------


MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kugawa nakala za vitabu viwili vinavyoelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020-2025 katika jimbo hilo.

Vitabu hivyo vinagawiwa bure kwa viongozi wa CCM wa ngazi zote, lakini pia kwa viongozi wa serikali na wananchi wengine ndani wa jimbo la Musoma Vijijini.

Prof Muhongo aligawa vitabu hivyo na simu mpya ya kuandikisha wanachama wa CCM katika kata ya Suguti wiki iliyopita.
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages