Na Mwandishi wa
Mara Online News
-----------------------------
Mara Online News
-----------------------------
WATU 685 wakiwemo watoto 384 wamekosa makazi baada ya nyumba zao kubomolewa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Lyasembe kilichopo kata ya Murangi, jimbo la Musoma Vijijini.
Maafa hayo yalitokea Ijumaa iliyopita, ambapo nyumba 17 zilibomolewa na nyingine 59 za wanakijiji kuezuliwa mapaa. Pia vyumba viwili vya madarasa ya Shule ya Msingi Lyasembe viliezuliwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa vyombo vya habari jana, pia miti mikubwa 28 iliyong'olewa na mingine 12 kuvunjiwa matawi.
Jana, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alifika kijijini Lyasembe kushuhudia maafa yaliyobabishwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.
Kutokana na hali hiyo, Prof Muhongo anashirikiana na Serikali ya Kijiji cha Lyasembe kuomba wadau wote wa maendeleo kujitokeza kutoa misaada ya aina mbalimbali, hususan vifaa vya ujenzi kama vile saruji, mabati, mbao na misumari kwa ajili ya kurejesha makazi ya waathirika wa maafa hayo.
No comments:
Post a Comment