NEWS

Tuesday 23 April 2024

Mafuriko Bonde la Mto Mara: Mashamba yajaa maji kijijini Matongo, viongozi waomba msaadaMuonekano wa sehemu ya shamba la mahindi lililojaa maji kijijini Matongo.
----------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News
---------------------------


MAMIA ya wananchi katika kijiji cha Matongo wilayani Tarime, Mara wako hatarini kukumbwa na baa la njaa kufuatia mashamba yao yakiwemo ya zao la mahindi kuathiriwa na mafukio.

Inakadiriwa kuwa mafuriko hayo yameathiri kaya zaidi ya 1,500 zilizopo kando kando ya Bonde la Mto Mara.

“Haya ni mafuriko na msimu uliopita pia hatukuvuna, cha kwanza tunaomba msaada wa chakula, cha pili tunaomba mbegu,” Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Matango, Daudi Itembe ameimbia Mara Online News kijijini hapo leo Aprili 23, 2024.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mara Online News wamesema hawana mategemeo ya kuvuna chochote baada ya mashamba yao kujaa maji.

“Tunategemea haya mahindi lakini sasa mashamba yamejaa maji, tuna watoto, hatujui watakula nini, tunaomba msaada,” amesema mkazi wa kijiji hicho aliyejitambuisha kwa jina la Maningo.


Kijiji cha Matongo kina idadi ya watu zaidi ya 7,000 ambao maisha yao hutegemea kilimo na ufugaji.

Mara Online News inaendelea na juhudi za kupata majibu ya mamlaka za serikali zenye dhamana ya kilimo na zinazokabiliana na maafa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages