NEWS

Thursday 18 April 2024

Rais Samia aweka wazi lengo la ziara yake nchini UturukiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki jana Aprili 17, 2024 kwa ajili ya ziara rasmi.
---------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan aliwasili nchini Uturuki jana Aprili 17, 2024 kwa ajili ya ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Rais Recep Erdoğan.

“Nimewasili nchini Uturuki kwa ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Rais Recep Erdoğan. Mwaka huu nchi zetu mbili zinatimiza miaka 45 tangu kuanza kwa uhusiano wetu wa kidiplomasia.

“Uturuki ni mshirika wetu mkubwa kiuchumi na ni soko la kimataifa kwa bidhaa zetu linalokua kwa kasi, tukiwa na ukubwa wa biashara baina yetu wa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 350 kwa mwaka.

“Ziara yangu ni sehemu ya utekelezaji wa sera yetu ya Mambo ya Nje kupitia Diplomasia ya Uchumi, katika kutafsiri uhusiano wetu na nchi nyingine uwe wenye kuleta tija na kuchangia ukuaji wa uchumi wetu,” Rais Samia aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.


Rais Dkt Samia akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Familia na Huduma za Jamii wa Uturuki, Mahinur Ozdemir Goktas mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki jana kwa ajili ya ziara rasmi.
--------------------------------------------------

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages