NEWS

Thursday 2 May 2024

Jenerali Kahariri ateuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Kenya, Meja Jenerali Fatuma naye Bosi wa Jeshi la AngaJenerali Charles Muriu Kahariri
------------------------------------------

RAIS William Ruto amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) ya Kenya.

Rais Ruto amefanya uteuzi huo, ikiwa ni wiki mbili zimepita baada ya Jenerali Francis Ogolla aliyekuwa CDF kufariki dunia katika ajali ya helikopta nchini humo.

Amempandisha cheo kutoka Luteni Jenerali kuwa Jenerali na kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Kahariri alikuwa Makamu wa CDF Jenerali Ogolla.


Rais William Ruto (kushoto) 
akimpandisha cheo Kahariri
------------------------------------------------

“Rais wa Jamhuri ya Kenya na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, kwa mujibu wa kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, leo amempandisha cheo Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri hadi cheo cha Jenerali na kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi," inaeleza taarifa hiyo.

Rais pia amempandisha cheo Meja Jenerali John Mugaravai Omenda hadi cheo cha Luteni Jenerali na kumteua kuwa Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.

Hadi kuteuliwa kwake, Luteni Jenerali Mugaravai alikuwa Kamanda wa Jeshi la Wanahewa la Kenya.

Wakati huo huo, Rais Ruto amemtuma Meja Jenerali Fatuma Gaiti Ahmed kwa Jeshi la Wanahewa (Anga) la Kenya na kumteua kuwa Kamanda wake.


Meja Jenerali Fatuma Gaiti Ahmed
----------------------------------------------

Fatuma Gaiti alikuwa mwanajeshi wa cheo cha juu zaidi wa kike mwaka wa 2015, baada ya Rais Uhuru Kenyatta (wakati huo) kumpandisha cheo hadi Meja Jenerali.

Kulingana na mabadiliko hayo, Ruto alimpandisha Meja Jenerali Paul Owuor Otieno kwa Wanamaji wa Kenya na kumteua kuwa Kamanda wa kitengo hicho.

Baadaye, kwa ushauri wa Baraza la Ulinzi, linaloongozwa na Waziri wa Ulinzi, Aden Duale, Rais Ruto alishikilia mapendekezo ya baraza hilo na kufanya mabadiliko hayo na uteuzi wa vikosi vya Ulinzi vya Kenya.
Chanzo: TUKO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages