NEWS

Wednesday 1 May 2024

Tanzania kushiriki Kongamano la Jukwaa la Maji DunianiWaziri wa Maji, Jumaa Aweso (kushoto) akiwa na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Tri Yogo Jatmiko walipokutana na kufanya mazungumzo jijini Dodoma jana.
-----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
----------------------------------------


WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amefanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Tri Yogo Jatmiko kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Kongamano la 10 la Jukwaa la Maji Duniani, litakalofanyika Mei 19 hadi 20, 2024 nchini Indonesia.

Mazungumzo hayo yalifanyika jijini Dodoma jana, ambapo Waziri Aweso aliiomba Indonesia kuisaidia Tanzania katika maeneo ya uwekezaji wa miradi mikubwa ya maji, kuwajengea uwezo wataalamu katika sekta ya maji, teknolojia ya upatikanaji wa dira za maji za malipo kabla (pre-paid meter) na katika eneo la uendelezaji wa rasilimali za maji.

Balozi Jatmiko alitumia nafasi hiyo pia kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukubali mwaliko wa kushiriki katika kongamano hilo la wadau wa sekta ya maji duniani, ambalo lina fursa nyingi katika uwekezaji kwenye sekta ya maji, utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Rais Dkt Samia atawakilishwa na Waziri Aweso katika kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages