NEWS

Thursday 30 May 2024

Matokeo ya kwanza yatangazwa uchaguzi Afrika Kusini 2024Matokeo ya kwanza yametangazwa katika uchaguzi ambao unaonekana kuwa ni uchaguzi uliopiganiwa kwa karibu zaidi nchini Afrika Kusini .
-----------------------------------------------

Matokeo ya kwanza yametangazwa ya uchaguzi unaoonekana kuwa wenye ushindani zaidi nchini Afrika Kusini tangu chama cha African National Congress (ANC) kiingie madarakani miaka 30 iliyopita.

Huku matokeo kutoka kwa zaidi ya asilimia 11 ya wilaya za wapiga kura yakiwa yamehesabiwa kufikia sasa, ANC inaongoza kwa 43%, ikifuatiwa na DA yenye 26%.

Chama chenye msimamo mkali cha EFF na Umkhonto weSizwe (MK Party) cha Rais wa zamani Jacob Zuma vina karibu 8%.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa mwishoni mwa juma.

Kura za maoni zinaonesha kuwa chama cha ANC kinaweza kupoteza wingi wake bungeni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30.

Chama cha ANC kimepoteza uungwaji mkono kutokana na hasira juu ya viwango vya juu vya rushwa, uhalifu na ukosefu wa ajira.

Lakini ni mapema sana kutabiri matokeo ya mwisho. Uchaguzi wa Alhamisi ulishuhudia misururu mirefu ya wapiga kura nje ya vituo vya kupigia kura hadi usiku wa manane kote nchini. 
Msururu mrefu wa raia wa Afrika Kusini ambao waliamka mapema wakisubiri kwa hamu zamu yao ya kupiga kura katika uchaguzi wa leo."
 
                                                  

 

Chanzo:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages