Na Mwandishi Wetu, Musoma
----------------------------------------
----------------------------------------
Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameipatia Timu ya UMITASHUMTA ya jimbo hilo msaada wa ‘track suits’ 100 na jezi 16.
Wanafunzi wa shule za msingi za jimbo la Musoma Vijijini walikabidhiwa msaada huo jana, na tayari wako kambini wakifanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Mara.
Timu ya UMITASHUMTA ya mpira wa miguu ikiwa mazoezini kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Suguti, jimbo la Musoma Vijijini.
----------------------------------------------------
Ilani ya Uchaguzi ya chama tawala - CCM ya Mwaka 2020-2025 inaelezea umuhimu wa michezo na utamaduni kwa Taifa letu.
Hivyo michezo na utamaduni ni moja ya vipaumbele vikuu vitano vya jimbo la Musoma Vijijini.
“Tunawatakiwa wanafunzi wetu ushindi mzuri kwenye mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Mara,” alisema Prof Muhongo.
No comments:
Post a Comment