NEWS

Wednesday 19 June 2024

Buriani RAS Tixon Nzunda

Tixon Tuyangine Nzunda enzi za uhai
----------------------------------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemtumia Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watumishi wake wawili.

Watumishi hao; Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) wa Kilimanjaro, Tixon Tuyangine Nzunda na dereva wake, Alphonce Edson walifariki dunia jana Juni 18, 2024 kwa ajali ya gari katika eneo la njiapanda ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wilayani Hai.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa, watumishi, familia, ndugu, jamaa na wananchi wote wa mkoa wa Kilimanjaro kutokana na vifo vya watumishi hao wa serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages