NEWS

Wednesday 10 July 2024

Askari Polisi wanne wafukuzwa kazi Kilimanjaro
Na Mwandishi Wetu
---------------------------

Jeshi la Polisi Tanzania limewafukuza kazi askari wake wanne wa kitengo cha usalama barabarani.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime ilisema askari hao walikuwa wakifanya kazi katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

“Baada ya uchunguzi kukamilika ilibainika kuwa askari hao walikuwa wamefuta picha kutoka kwenye camera za Jeshi la Polisi walizokuwa wanatumia kupima mwendo kasi wa madereva waliokuwa wanakiuka sheria za usalama barabani kwa maslahi yao binafsi.

“Walishtakiwa kijeshi na wakapatikana na hatia, na Julai 8, 2024 walifukuzwa kazi na kufutwa jeshini,” ilihitimisha taarifa hiyo bila kutaja majina ya askari hao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages