NEWS

Tuesday 9 July 2024

Aliyekuwa RC Simiyu apandishwa kizimbani Mwanza
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
---------------------------------------

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (RC) wa Simiyu, Dkt Yahaya Nawanda, leo amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka la kumlawiti mwanamke mwenye umri wa miaka 21.

Dkt Nawanda amesomewa shtaka hilo na Waendesha Mashtaka wa Serikali, Magreth Mwaseba na Martha Mtiti, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Mwanza, Erick Maley.

Waendesha Mashtaka hao wameieleza mahakama kwamba Dkt Nawanda alitenda kosa hilo Juni 2, 2024 katika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza, kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Hata hivyo, Dkt Nawanda alikana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya mahakama ya kuwa na wadhamini wawili [mmoja mtumishi wa umma na mwingine wa sekta binafsi] na mali isiyohamishika yenye thamani isiyopungua shilingi milioni tano.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 16, 2024 ambapo mshtakiwa huyo atasomewa maelezo ya awali, kabla ya usikilizaji kuanza, na upande wa mlalamikaji umetakiwa kupeleka mashahidi siku hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages