CEO wa Mara Online, Jacob Mugini (mwenye kaunda suti ya kaki) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Afya Magena wakati wa maadhimisho ya Siku Maalumu ya kituo hicho jana Julai 13, 2024. (Picha na Mara Online News)
-------------------------------------------------
----------------------------------------
Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mara Online, Jacob Mugini ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Kituo cha Afya Magena kilichopo kilomita chache kutoka mji wa Tarime.
Sherehe za maadhimisho hayo zilifanyika kituoni hapo jana Julai 13, 2024, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Maulid Surumbu.
Kituo hicho kipo jirani na Uwanja wa Ndege Magena unaotumiwa na ndege nyingi za watalii wanaokweda kutembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti, mashariki mwa wilaya ya Tarime.
“Hongereni sana, Kituo cha Afya Magena mnasifika kwa kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi,” CEO Jacob ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara aliwapongeza wafanyakazi wa kituo hicho.
Magena ni miongoni mwa vituo vya afya vya serikali vilivyopo katika Halmashauri ya Mji wa Tarime, mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment