Donald Trump akioonekana pichani na jeraha la risasi sikioni huku walinzi wake wamemzunguka kumwekea ulinzi
--------------
--------------
Milio inayokisiwa kuwa risasi imesikika kwenye mkutano wa hadhara wa Donald Trump huko Pennsylvania wakati rais huyo wa zamani alipokuwa akitoa hotuba.
Alikimbizwa nje ya jukwaa haraka na maafisa wa kitengo cha Secret Service.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alitolewa nje ya jukwaa baada ya milio ya risasi kuzuka katika mkutano wa hadhara huko Pennsylvania katika jaribio la kutaka kumuua.
Picha zilimuonyesha akiwa na hasira na kuinua mkono kwenye sikio lake la kulia, kabla ya kuinama -huku mfululizo wa milio ya risasi ikisikika.
Upesi alivamiwa na maajenti wa Huduma ya Secret Service wanaomlinda na kuvutwa kutoka jukwaani hadi kwenye gari linalomsubiri. Aliinua ngumi huku akiingizwa kwenye gari.
Katika chapisho kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema risasi ilipenya "sehemu ya juu" ya sikio lake la kulia. Hapo awali, msemaji wake alisema "anaendelea vizuri" na anapokea matibabu katika kituo cha matibabu cha eneo hilo.
"Nilijua mara moja kuwa kuna kitu kibaya kwa kuwa nilisikia sauti ya mlio, milio ya risasi, na mara moja nikahisi risasi ikipasua kwenye ngozi," Trump aliandika. "Nilivuja damu nyingi, kwa hivyo niligundua kile kinachotokea."
Damu zilionekana wazi kwenye sikio na uso wa Trump huku maafisa wa ulinzi wakimkimbiza.
Mshukiwa huyo alipigwa risasi na kufa katika eneo la tukio na maafisa wa Secret Service, msemaji wa shirika hilo Anthony Guglielmi alisema. Aliongeza kuwa mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment