NEWS

Sunday, 14 July 2024

Tarime Sekondari yang'ara tena Matokeo ya Mtihani Kidato cha Sita




Na Mwandishi Wetu
---------------------------

Shule ya Sekondari Tarime imeng’ara tena katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita kwa Mwaka 2024 baada ya wanafunzi wake 355 kupata ufaulu wa daraja la kwanza (A).

Kwa mujibu wa matokeo hayo ambayo yalitangazwa jana na kuchapishwa kwenye tovuti ya Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA), wahitimu wengine 96 wa shule hiyo wamepata ufaulu wa daraja pili (B) na watatu wamepata daraja la tatu (C).

Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa katika Matokeo ya Kidato cha Sita Mwaka jana (2023), kati ya wanafunzi 498 wa Sekondari ya Tarime waliofanya Mtihani wa Taifa wa kuhitimu kidato hicho, 357 walipata ufaulu wa daraja la A na 130 walipata darala B.

Shule hiyo ambayo ipo katika Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara, imeendelea kuweka rekodi ya juu katika matokeo ya kidato cha sita kwa miaka kadhaa mfulilizo.

Shule ya Sekondari Tarime ambayo pia imefanyiwa ukarabati mkubwa na Serikali ya Tanzania, inapokea wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Matokeo hayo ya Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Sita na Ualimu kwa Mwaka 2024 yalitangazwa juzi Jumamosi na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt Said Ali Mohamed katika Ofisi za Baraza hilo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages