
Kikosi cha timu ya Hispania wakifurahia ushindi wao wa Euro 2024 baada ya Kuinyuka Uingereza 2-1
-------------
Hispania ilishinda michezo yote saba bila kuhitaji mikwaju ya penati, rekodi mpya katika Mashindano ya Ulaya. Ushindi wa 2-1 dhidi ya Uingereza katika fainali uliwafanya kuwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya nne.
Walipata ushindi kwa njia ngumu, wakishinda mataifa mengine yote ya Ulaya ambayo yamewahi kushinda Kombe la Dunia - Italia, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, pamoja na Croatia waliofika fainali mwaka 2018 - kuelekea ushindi wao huko Berlin.
Rodri alikuwa mchezaji bora wa mashindano. Lamine Yamal alikuwa mchezaji mdogo bora. Dan Olmo alishinda tuzo ya kiatu cha dhahabu ‘Golden Boot’. Yamal alikuwa na msaada mkubwa katika kupatikana kwa magoli ya timu yake ya Taifa kwa maana ya kutoa ‘assist’ nyingi
Hata kocha wa Uingereza, Gareth Southgate, alikubali kwamba Hispania walistahili kuwa mabingwa.
"Hongera Hispania. Walistahili kushinda sio tu usiku huu, bali katika mashindano yote," aliongeza kocha wa Uingereza
CHANZO: BBC NEWS
No comments:
Post a Comment