NEWS

Monday, 15 July 2024

Rais Samia avutiwa Hifadhi ya Katavi, aahidi kufanya ‘royal tour’ ya kuitangaza



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi leo.
-----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Katavi
-------------------------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amevutiwa na wanyamapori mbalimbali katika Hifadhi ya Taifa Katavi, na kuahidi kufanya filamu nyingine ya ‘Royal Tour’ kwa ajili ya kuitangaza hifadhi hiyo.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi, baadaya kutembelea hifadhi hiyo leo Julai 15, 2024.

Ametoa ahadi hiyo kujibu ombi la Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda aliyeomba Royal Tour nyingine ifanyike mkoani humo.

Swala ndani ya Hifadhi ya Taifa Katavi
------------------------------------------------

“Nataka nikiri kwamba zile sifa alizozisema Waziri Mkuu Mstaafu kuhusu uwepo wa wanyama wengi na wa kuvutia katika Hifadhi ya Katavi, nimeziona mwenyewe na zimetimia maana leo nilipita kwenye mbuga hiyo kuona ikoje, mahitaji yakoje.

“Tumeona mambo mengi ya kufanya mle ndani na suala la Royal Tour, Waziri wa Maliasili na Utalii ameshaandika, hivyo jipange na ukiwa tayari mimi mwenyewe nitakuja,” amesema Rais Samia.

Baadhi ya mawaziri walioambatana na Rais Samia katika ziara hiyo wakifuatilia jambo.
----------------------------------------------

Kiongozi huyo wa nchi amekuwa katika ziara mkoani Katavi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na leo ameingia mkoani Rukwa kuendelea na ziara hiyo.

UNAWEZA PIA KUSOMA:

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages