
Aliko Dangote
--------------------
Tajiri mkubwa barani Afrika, Aliko Dangote amewashangaza watu wengi wa Nigeria, baada ya kusema hana nyumba nje ya nchi hiyo.
Dangote alisema alikuwa na nyumba mbili - katika mji aliozaliwa wa Kano, na Lagos - na aliishi katika nyumba ya kukodi kila anapotembelea mji mkuu, Abuja.
Aliorodheshwa na jarida la Forbes Januari 2024 kama mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mwaka wa 13 mfululizo, licha ya matatizo ya kiuchumi nchini humo.
Utajiri wake ulipanda kwa dola milioni 400 zaidi mwaka 2023, na kumpa thamani ya jumla ya dola bilioni 13.9, Forbes walisema wakati huo.
Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 66, alijitajirisha kwa saruji na sukari - na mwaka 2023 alifungua kiwanda cha kusafisha mafuta katika kitovu cha uchumi cha Nigeria, Lagos.
Dangote alibainisha hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote juzi Jumapili.
Maoni yake yaliwashangaza wengi katika nchi ambayo watu matajiri wana sifa ya maisha ya kifahari.
Wanigeria wengi matajiri wanamiliki nyumba London, Dubai na Atlanta.
Matamshi yake yamezua hisia nyingi kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakisema ni uamuzi wa busara wa kibiashara kwani ni nafuu kulipa kodi kuliko kununua nyumba.
Dangote alisema sababu ya uamuzi wake ni kwamba anataka kuona Nigeria inakua.
“Sababu ya kutokuwa na nyumba London au Marekani ni kuwa nilitaka kuangazia ukuaji wa viwanda nchini Nigeria,” alisema.
“Nina shauku kubwa juu ya ndoto ya Nigeria na kando na nyumba yangu ya Lagos, nina nyumba nyingine katika jimbo langu la Kano, na nyingine ya kukodi huko Abuja.
“Ikiwa nitakuwa na nyumba kote Marekani na kwingineko, nisingeweza kutuliza akili na kufanya kitu kwa ajili ya watu wangu.”
Dangote anajulikana kumiliki makazi ya kifahari katika Kisiwa cha Banana maarufu cha Lagos, ambako Wanigeria wengi wenye hadhi ya juu pia wana majumba ya kifahari.
Mchambuzi wa masuala ya umma, Sani Bala alisema Dangote alikuwa akionesha mfano mzuri sana.
“Wanaigeria wanahitaji kuelekezwa upya kuelewa kumiliki majumba kadhaa sio mafanikio wakati pesa zingehitajika mahali pengine.
“Dangote alisema aliuza nyumba yake huko London mwaka 1996, na nina uhakika pesa zilizopatikana kutokana na mauzo zilirejeshwa katika biashara yake, huo ndio mfano wa kuiga,” alisema Sani. BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
-
>>1. Mamlaka zanasa watuhumiwa wawili, magunia 205 ya dawa za kulevya Mara >>
2.>>Mwenyekiti UVCCM Mara: Sauti ya Mara mnafanya vizuri kutangaza habari chanya za wawekezaji waliopo ndani ya mkoa >>
3.>>Simiyu: Wananchi wazuia mabasi ya abiria Nyamikoma, baadhi yadaiwa kupondwa mawe >>
4.>>Tarime Sekondari yang'ara tena Matokeo ya Mtihani Kidato cha Sita
>>5.Hispania yashinda Euro tena kwa mara ya nne
>>6. Mamlaka zanasa watuhumiwa wawili, magunia 205 ya dawa za kulevya Mara >>6.Rais Samia avutiwa Hifadhi ya Katavi, aahidi kufanya ‘royal tour’ ya kuitangaza
No comments:
Post a Comment