NEWS

Thursday 11 July 2024

Wachezaji 9 wenye asili ya Afrika wanaong'aa EURO 2024Mashindano ya EURO 2024 yamefikia hatua ya fainali, ambapo England itachuana na Spain. Vijana wadogo wameonesha uwezo mkubwa, wengine wakiwa na asili ya Afrika.

Tangu mashindano yaanze, baadhi ya wachezaji wenye asili ya Afrika wanafanya vyema. Wachezaji hao wangekuwa na uwezo wa kucheza nchi fulani barani Afrika.

Wafuatao hapa chini ni baadhi ya wachezaji wanaofanya vizuri hadi sasa kwenye michuano hiyo ya EURO inayofanyika Ujerumani.

Jamal Musiala
Jamal Musiala kutoka klabu ya Bayern Munich, alizaliwa Ujerumani. Ni kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 21, tayari yuko kwenye chati ya wafungaji mabao akiwa na mabao 3. Ni mmoja wa wachezaji muhimu wa Ujerumani.
Jamala Musiala ana asili pana sana. Angeweza kuichezea England, Nigeria, au Poland. Baba yake ana asili ya Nigeria na Uingereza, na mama yake ni Mjerumani mwenye asili ya Poland.

Jamine Yamal
Huyu ni winga wa Barcelona aliyepata umaarufu baada ya kocha Xavi Xernandez kumpa nafasi ya kuchezea timu ya wakubwa.
Yamal amekuwa aking'ara katika klabu yake na hadi timu ya taifa akiwa na miaka 16.

Katika msimu wa 2023/24 amecheza michezo 50 kwa Barcelona katika mashindano yote.

Katika michuano ya EURO, winga huyu ni mmoja wa wachezaji muhimu wa kocha wa Uhispania, Luis de la Fuente.

Kijana huyu amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza mechi ya EURO, na kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika michuano hiyo.

Yamal anafaa kuchezea Morocco, au Guinea ya Ikweta, asili ya wazazi wake - lakini amechagua Uhispania kwa kuzaliwa.

Nico Williams
Nico Williams ni ndugu wa mchezaji wa Athletic Bilbao na mshambuliaji wa Black Stars, Inaki Williams ambaye aliamua kuichezea Ghana Agosti 2022.
Lakini kaka yake mdogo Nico Williams ambaye pia anastahili kuichezea Ghana, aliamua kuichezea Uhispania, kutokana na kuzaliwa huko.

Nico akitafakari safari ya wazazi wake kutoka Ghana had Uhispania anasema, “Namshukuru Mungu kwamba tuko pamoja sasa na maisha ni mazuri. Wazazi wangu wanatazama watoto wao waking’aa - kila kitu tunachofanya ni kwa ajili ya wazazi wetu.”

Katika michuano ya EURO, Nico ni mmoja wa wachezaji bora wa Uhispania.

Tetesi zimeibuka kwamba Barcelona wanataka kumsajili mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 21.

Kylian Mbappe
Baba yake Mbappe ni kutoka Cameroon na mama yake ana asili ya Algeria.
Mbappe, mshambulizi wa zamani wa PSG, ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani, na ana mizizi barani Afrika.

Julai 2023, alipotembelea Yaounde, alisema: "Ni heshima kuwa pamoja na familia yangu na kuonana na marafiki wote ambao wanaonesha upendo mwingi."

"Nina mipango na miradi mingi kwa ajili ya Cameroon kwa watoto na kwa siku zijazo," Mbappe aliwambia waandishi wa Habari.

Mbappe aliyejiunga na Real Madrid amefunga bao moja na ametoa pasi moja iliyosababisha bao. Tayari timu yake ya Ufaransa imeomndolewa katika michunao hiyo baada ya kusachapwa mabao 2-1 na Uhispania katika mechi ya nusu fainali.

Kwadwo Antwi Duah
Kwadwo aliifungia Switzerland dhidi ya Hungary katika mchezo wa ufunguzi. Ni mshambulizi mwenye umri wa miaka 27 anayechezea klabu ya Ludogoretz ya Bulgaria.
Alizaliwa London na wazazi wake kutoka Ghana mwaka 1997. Ni mmoja wa wachezaji watatu waliofunga kwenye mechi ya kwanza katika Timu ya Taifa ya Switzerland.

Baada ya mchezo huo alisema: "Huu ni mchezo wangu wa pili wa kimataifa, na nimefunga bao langu la kwanza - ninafuraha sana.”

Katika majira ya kiangazi ya 2022, alipokea mwaliko kutoka Chama cha Soka cha Ghana kucheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia la 2022 dhidi ya Nigeria, lakini alikataa ofa hiyo.

Breel Embolo
Embolo anachezea Monaco, aliifungia Switzerland bao la 3 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Hungary.
Familia ya Embolo ni asili ya Cemeroon. Katika Kombe la Dunia la Mwaka 2022, Embolo hakusherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya Cameroon.

Tangu alipocheza kwa mara ya kwanza mwaka 2015, sasa amecheza mechi 60 kwa Switzerland, na anatazamia kucheza zadi EURO.

Embolo mwenye umri wa miaka 27, anatembelea Cameroon kwa ajili ya likizo na pia familia na marafiki.

Manuel Obafemi Akanji
Akanji ana mama wa Switzerland na baba kutoka Nigeria. Baba yake pia alicheza mpira.
Akanji alisema: “Nchini Nigeria, nataka kuwasaidia watoto ambao hawajapata bahati kama niliyo nayo mimi nchini Uswizi.”

Mlinzi huyo wa Manchester City, anasema Burna Boy ndiye msanii anayempenda zaidi.

Ni mchezaji muhimu wa Timu ya Taifa ya Switzerland.

Bukayo Saka
Huyu alizaliwa na wazazi kutoka Nigeria. Ni winga wa Arsenal anayeiwakilisha England katika ngazi ya vijana na timu kubwa pia.
Shirikisho la Soka la Nigeria halijajaribu kumleta Saka lakini haiwezekani kufanya hivyo baada ya kucheza katika timu ya vijana nchini Uingereza.

Saka amefanya vyema ndani ya Arsenal msimu uliopita kiasi kwamba mashabiki wa England wanatumai ataibuka kuwa mfungaji bora katika michuano ya EURO.

Jeremy Frimpong
Jeremy Frimpong ni mmoja wa wachezaji muhimu wa Bayer Leverkusen, iliyoshinda taji akiwa na mabao 8 msimu uliopita.

Ana umri wa miaka 23, amecheza michezo 31 katika klabu yake kabla ya kocha wa Uholanzi, Ronald Koeman kumwita kwa ajili ya EURO.

Chama cha Soka cha Ghana kilimwita Frimpong lakini alikataa mwaliko wa kuichezea Ghana.

“Kocha wa Ghana alinipigia simu mwaka 2023, lakini nia yangu ni kuichezea Uholanzi,” anasema.

Tayari timu yake ya Uholanzi imeondolewa katika mashindano hayo baada ya kufungwa mabao 2-1 na England katika mechi ya nusu fainali jana Jumatano. BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages