NEWS

Saturday, 14 December 2024

Filamu ya `Tantalizing Tanzania` yazinduliwa India kukuza utalii wa Tanzania



Na Mwandishi Wetu

Jiji kubwa la kibiashara la Mumbai nchini India Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyopita lilishuhudia kuzinduliwa kwa filamu ya kuvutia inayotangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

Filamu hiyo inayoitwa “Tantalizing Tanzania” inamhusisha mwanamuziki mashuhuri wa India, Shakti Mohan, ambaye amepiga picha mjongeo katika hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na visiwa vya Zanzibar.

Filamu hiyo, iliyoandaliwa na kampuni ya kuwahudumia watalii wa India na Tanzania ya Swahili Safari,ilizinduliwa na Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt Pindi Chana, na Waziri mwenzake wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soraga, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India.




Uzinduzi huo wa filamu ulishuhudiwa na mfanyabiashara, mchapishaji na mwandishi maarufu wa vitabu wa Tanzania, Nyambari Nyangwine, ambaye ni miongoni mwa wadau waliodhamini tukio hilo kupitia taasisi yake ya Nyambari Nyingwine Foundation.

Mmiliki wa kampuni ya Swahili Safari iliyoandaa uzinduzi wa filamu hiyo ni rafiki wa karibu wa mfanyabiashara huyo wa Tanzania.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages