NEWS

Sunday, 15 December 2024

Kibu 'Mkandaji' atakata Simba ikiwachapa Watunisia 2-1



Kibu Dennis Prosper (katikati) na wachezaji wenzake wakifurahia ushindi.
------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Mchezaji wa Simba SC, Kibu Dennis Prosper - maarufu kama 'Mkandaji' ameiwezesha timu yake kuibuka na alama tatu muhimu baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika mechi ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kibu amefunga magoli yote mawili kwa kichwa, ambapo aliweka goli la kwanza dakika ya saba ya mchezo, kisha akafunga goli la pili katika dakika za nyongeza na kuwapa furaha mashabiki wa wekundu hao wa msimbazi.


Kufuatia ushindi huo, Simba sasa imefikisha jumla ya alama sita zinazoifanya timu hiyo kushikilia nafasi ya pili katika msimamo wa kundi A, huku matumaini yao ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali yakiongezeka.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages