NEWS

Sunday, 5 January 2025

Heche amchoka Mbowe uenyekiti CHADEMA, atangaza kumuunga mkono Lissu



John Heche

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, John Heche ameweka hadharani msimamo wake wa kumuunga mkono Tundu Lissu katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama hicho.

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa upande wa Bara, atachuana na Freeman Mbowe anayetetea nafasi hiyo katika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho ngazi ya taifa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu wa Januari 2025.

Wakati huo huo, akiwa jijini Mwanza, Heche ambaye wamewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini mwaka 2015-2020, ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Bara) katika uchaguzi huo.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages