NEWS

Monday, 6 January 2025

Makundi maalum Musoma Vijijini yajazwa mikopo ya shilingi milioni 400




Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, vimepata mikopo ya shilingi milioni 400 iliyotolewa na halmashauri hiyo kuviwezesha kuendesha miradi ya kiuchumi ili kuboresha maisha.

Hafla ya utoaji wa mikopo hiyo isiyokuwa na riba ilifanyika hivi karibuni kijijini Suguti yalipo makao makuu ya halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Issa Chikoka.

Viongozi mbalimbali, akiwemo Mbunge wa Musoma jimbo la Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, pia walihudhuria hafla hiyo.

Hivi sasa, wilaya ya Musoma ya mkoani Mara imesimama kidete kutekeleza miradi mbalimbali ya kuwasaidia wananchi kuondokana umaskini.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages