NEWS

Friday, 2 May 2025

Ajali yakatisha maisha ya Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tarime



Felix Ngoda enzi za uhai

Na Joseph Maunya, Tarime

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara, Felix Ngoda, amefariki dunia baada ya kupata ajali ya pikipiki mjini humo jana Mei 1, 2025.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Gimbana Ntavyo, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mtumishi wake na kwamba taarifa za tararibu za mazisha zitatolewa.

Mara Online News inaendelea na juhudi za kumpata Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime - Rorya kwa ajili ya kuzungumzia zaidi tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages