NEWS

Saturday, 24 May 2025

Mara Intercultural Festival yazinduliwa Rorya



Mkurugenzi wa Kampuni ya Grace Entertainment and Promotion, Grace Revocatus, akizungumza katika uzinduzi wa Mara Intercultural Festival wilayani Rorya jana Mei 23, 2025. (Picha na Mara Online News)
------------------------------------

Na Agnes Kajana, Rorya

Kampuni ya Grace Entertainment and Promotion imezindua tamasha la Mara Intercultural Festival yanayolenga kuwaleta wana-Mara pamoja na kutangaza utamaduni wa mkoa huo.

Uzinduzi huo ulifanyika Shirati wilayani Rorya jana Mei 23, 2025 na kuhusisha michezo na huduma mbalimbali.
“Tunatangaza tamaduni na mila zetu za mkoa wa Mara kwa kutumia makabila yote yaliyopo, tunatembea kila wilaya ambapo kila kabila litapata nafasi kutoa mshiriki kwa ajili ya kushindana kimkoa,” Mkurugenzi wa Grace Entertainment and Promotion, Grace Revocatus, alisema.

Kwa upande wake, Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Said Masanja, alimpongeza Mkurugenzi Grace akisema tamasha hilo ni fursa kubwa kwa ajili ya kuibua vipaji vya sanaa kwa vijana.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Mara, Ngoja Msangia Ongoti, alisema matamasha ya aina hiyo yatasaidia pia kuimarisha umoja wa makabila ya mkoa huo.

“Muda mwingi tumepuuza tamaduni zetu, lakini sasa hatua hii itasaidia kuufufua upya, kila jamii na mtu mwenye talanta ya mila na desturi, mchezo na mambo yetu ya asili tunataka yawe wazi,” alisema Ongoti.

Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Grace Entertainment and Promotion, Frank Lucas Salu, alieleza kufurahishwa na mwitikio mkubwa wa wananchi waliojitokeza katika tamasha hilo.

Mmoja wa wananchi waliohudhuria tamasha hilo aliwashauri vijana kuwa tayari kujitokeza kwa wingi katika matamasha kwa ajili ya kuonesha vipaji walivyonavyo.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages