NEWS

Thursday, 22 May 2025

Rais Mwinyi ajitolea kulipa gharama za uwanja mechi ya Simba dhidi ya Berkane



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto), akisalimiana na Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, mbele ya wachezaji wa timu hiyo.
-------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Klabu ya Simba "Wekundu wa Msimbazi" imemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kujitolea kulipa gharama zote za kutumia uwanja wa New Amaan Complex kwa ajili ya mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAFCC) dhidi ya RS Berkane ya Morocco itakayochezwa Mei 25, 2025.

Hatua hiyo ya Rais Mwinyi kubeba gharama hizo imetajwa kuwa ni zawadi maalum kwa Simba inayolenga kuhamasisha ushindi kwa klabu hiyo katika mchezo huo wa kihistoria, na kuunga mkono maendeleo ya michezo nchini.

Pamoja na kulipia gharama zote za uwanja na maandalizi ya mchezo huo, pia Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuhudhuria uwanjani hapo sambamba na Watanzania wengine ili kushuhudia mchezo huo mkubwa zaidi kuwahi kuchezwa visiwani Zanzibar kwa ngazi ya vilabu.

Simba inaingia kwenye mchezo huo wa pili wa fainali ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa magoli 2 - 0 kwenye mchezo wa kwanza wa uliochezwa nchini Morocco Mei 17, 2025 na sasa itahitaji ushindi wa kuanzia magoli 3 - 0 ili kupindiua meza na kutwaa taji hilo.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages