
Na Godfrey Marwa, Tarime
Umoja wa Wahitimu wa Zamani Shule ya Sekondari Mogabiri iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara umeipatia shule hiyo msaada wa kompyuta 10 na kompyuta mpakato moja ili kuinua kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, mwakilishi wa Mwenyekiti wa Umoja huo, Tumaini Jonathan Mwambara, alisema wamechukua hatua hiyo kurudisha shukrani zao shuleni hapo.
"Tumeona ni vyema kurudisha kidogo kwa shule iliyotufanikisha. Msaada huu utasaidia kuinua kiwango cha elimu ya TEHAMA, kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kidijitali, kuwaandaa vyema katika soko la ajira na dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa.
“Tunaahidi kuendelea kushirikiana na shule hii, na tunatoa wito kwa wahitimu wengine kujitokeza kushiriki katika juhudi hizi za maendeleo," alisema Mwambara.

Afisa Elimu kata ya Ketare, Bestina Subi, alishukuru akisema: "Niwashukuru sana wanafunzi waliowahi kusoma hapa - wamekumbuka nyumbani, msiishie hapo. Wanafunzi mnahitaji kusoma kwa bidii."
Naye Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Magudira Mugeta, aliushukuru umoja huo na kuuomba kuendelea na moyo huo wa upendo na kujitolea.
"Nawashukruni sana, msichoke kusaidia tena kwa sababu manufaa mliyonayo mmeyapata hapa Mogabiri Sekondari. Nawakaribisha mje mara nyingine ili Mogabiri yetu tuendelee kuiinua," alisema.
Nao wanafunzi wa shule hiyo walishukuru na kuahidi kusoma kwa bidii, na kutunza vifaa hivyo kwa manufaa yao na watakaofuata.



Unaweza pia kusoma:
»Tarime Vijijini: Nyambari achangia milioni 5/- ujenzi Kanisa Katoliki Kitenga, aungwa mkono na madiwani 20 – zapatikana milioni 11/-
»TAMISEMI yatoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano, vyuo vya kati 2025
»Waitara azishukia kamati za siasa CCM Musoma Mjini na Tarime, atamani zifutwe
No comments:
Post a Comment