
Mwita Waitara
Na Mwandishi Wetu, Musoma
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara na wadaiwa wenzake wawili wamehukumiwa adhabu ya kumlipa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba, Eliakim Maswi, fidia ya shilingi bilioni sita,
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Mahakama Kuu Kanda ya Musoma baada ya kumtia hatiani Mbunge Waitara kwa makosa ya kumkashifu na kutoa tuhuma za uongo dhidi ya Maswi alipokuwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi ya Umma (PPRA).
Shauri hilo Namba 23 la Mwaka 2023 lililofunguliwa na Maswi akitaka alipwe shilingi bilioni 12 kama fidia ya madhara ya jumla na shilingi bilioni moja kama fidia ya adhabu kwa madai ya kukashifiwa na kuzuliwa tuhuma za uongo za wizi wa fedha za serikali.
Pamoja na adhabu ya fidia iliyotolewa kwa wadaiwa hao; Waitara, Karoli Jacob na Mara TV, mahakama pia imewataka waitishe mkutano wa vyombo vya habari ili kumsafisha Maswi dhidi ya tuhuma walizotoa.
Mahakama pia imemtaka Waitara na wenzake walipe gharama zote za kesi.
No comments:
Post a Comment