NEWS

Tuesday, 17 March 2026

TRA Tarime yagawa bidhaa za magendo kwa taasisi za umma




Na Godfrey Marwa
Tarime
---------------

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara kupitia mpaka Sirari wilayani Tarime, leo Machi 17, 2026 imegawa bidhaa mbalimbali za viwandani kwa taasisi za umma.

Kwa mujibu wa TRA, bidhaa hizo ikiwemo saruji, mbolea, taulo za kike na vifaa tiba, ni miongoni mwa zilizokamatwa maeneo mbalimbali ya mpakani hapo kutoka kwa wafanyabiashara waliozivusha kwa kutumia njia zisizo rasmi (magendo) ili kukwepa kodi.


Kiondo akikabidhi mabomba ya sindano kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Deodat George.

Afisa Mfawidhi wa Forodha Kituo cha Sirari, Pascal Kiondo, amesema Kamishna wa Forodha ana mamlaka ya kisheria ya kugawa bidhaa hizo, hasa kwa taasisi za umma kama vile shule na hospitali.

"Tunaendelea kuwaasa siku zote wafuate taratibu za kiforodha ambazo ziko wazi na ni rahisi, endapo mtu anaona kuna ugumu wowote sisi kama Mamlaka milango ipo wazi kwa ajili ya kuwapatia elimu na kung’amua pale ambazo panaweza kuwa na shida,” amesema Kiondo.


Kiondo akigawa saruji

Naye Afisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Lepapa Lomnyaki Mollel, akipokea sehemu ya mbolea, ameishukuru TRA na kuahidi kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

"Nitoe shukrani zetu kwa TRA, mbolea hii tutaenda kuitumia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Mara, hasa katika mashamba darasa,” amesema Mollel.


Kiondo akimkabidhi Mollel mbolea

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages