Picha kutoka eneo la ajali |
Na mwandishi wetu, Tarime
Watu sita wamekufa papo hapo leo mchana katika ajali
ya gari ambayo imetokea eneo la
mteremiko wa Nyamwaga jirani na mgodi wa
North Mara Wilayani Tarime.
Aidha watu wengine 8 wamejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo
.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya limetibithisha vifo sita na majeruhi nane lakini inahofiwa kuwa idadi ya vifo inaweza kuwa zaidi ya sita
Ajali imehusisha gari la abiria aina hiace ambalo lilikuwa linaelekea Mugumu Wilayani Serengeti.
Ajali imehusisha gari la abiria aina hiace ambalo lilikuwa linaelekea Mugumu Wilayani Serengeti.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema gari hilo
lilipoteza uwelekeo na kutumbukia kwenye korongo.
Tutaendelea kukupatia taarifa zaidi kuhusu ajali hii.
Poleni sana wafiwa, mbele ya nyuma yetu
ReplyDelete