NEWS

Thursday 18 July 2019

BURUNDI YASHINIKIZWA NA WADAU KUHESHIMU UHURU WA HABARI

Picha ya Rais wa Burundi Pierre Nkuruzinza



Wanaopigania uhuru wa habari wanaweka shinikizo zaidi dhidi ya Burundi, baada ya makatazo kuongezeka ikipelekea Shirika la Habari la Uingereza BBC kufunga ofisi ya mwakilishi wake katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati wiki hii.
Serikali ya Burundi pia ilisitisha shirika la habari la VOA kufanya shughuli zake nchini humo tangu mwezi Machi 2019 na kutishia kuweka vikwazo dhidi ya kituo cha habari cha Radio France International.
Waandishi wa habari bila mipaka wameandika Jumatano kuwa “imepata wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya uhuru wa habari na kuwepo kwa vyama vingi nchini Burundi katika mchakato wa uchaguzi wa mwakani.”
“Ni idadi gani ya vyombo vya habari huru vitaachwa nyuma wakati Burundi itakapofanya uchaguzi wa rais mwaka 2020?,” kikundi hicho kimedadisi.
Ernest Sagaga, Mkuu wa haki za binadamu na usalama wa Muugano wa Waandishi wa habari wa Kimataifa ameiambia VOA kuwa uamuzi wa BBC kufunga ofisi zake unaonyesha kuwa BBC imetambuwa hivi sasa kuwa Burundi haina dhamira ya kuheshimu uhuru wa habari.”
Serikali ya Burundi haikupokea simu ya VOA wakati ikijaribu kupata maoni yao juu ya uamuzi wa BBC.
Kusitishwa kwa matangazo ya BBC, VOA
Mhariri wa BBC Afrika Will Ross amesema Jumanne kuwa shughuli za ofisi zitasimama “hadi hapo itakapotolewa taarifa zaidi” baada ya mazungumzo kati yake na serikali kurejesha operesheni za BBC kushindwa kufikia ufumbuzi.
Mnamo Machi 29, 2019, Bodi ya Mawasiliano ya Taifa nchini Burundi ilitoa katazo la mashirika ya habari ya Uingereza BBC na Sauti ya Amerika (VOA) kutorusha matangazo yake katika nchi hiyo.
Serikali hiyo pia ilipiga marufuku mtu yeyote kutoa taarifa ya aina yoyote kwa vyombo viwili hivyo vya habari.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages