Mbunge wa Viti Maalumu , Amina Makilagi(CCM) ametoa msaada wa kompyuta na printa vyenye thamani ya zaidi shilingi milioni tano kwa Jumuiya ya umoja wa Wanawake(UWT) Wilaya ya Tarime ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mbunge huyo alikabidhi msaada huo jana katika ofisi za CCM Wilaya ya Tarime ambapo alisema UWT ina kazi kubwa ya kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuaminika kwa wananchi.
"Sisi wanawake tukiamua tunaweza kama tulindavyo familia zetu basi tuweza kutilia mkazo suala la uhai wa chama pamoja na kuhakikisha tunajitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama"alisema Amina.
Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime Mkaruka Kura alimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo na kuahidi kuwa vifaa hivo vitatunzwa na kutumika vizuri.
No comments:
Post a Comment