NEWS

Saturday 27 July 2019

MARA DAY KUFANYIKA SERENGETI, SEPTEMBA 15Wanafunzi wakiimba nyimbo za uhifadhi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya mto Mara iliyofanyika Tanzania kwa Mara ya Kwanza , Mugumu Serengeti Septemba 15 ,2013
Na Mwandishi wetu, Serengeti
Sherehe za maadhimisho ya   siku ya Mto Mara mwaka huu zitafanyika nchini Tanzania Septemba 15  katika Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara .
 Tayari tumenaza maandalizi  na tunategemea  kupata wageni wengi kutoka  ndani na je ya nchi  watakaohudhuria  sherehe siku hii muhimu ,  Mkuu wa Wilaya ya Serengeti(DC) Nurdin Babu ameiambia Mara Online leo .
Tanzania na Kenya huadhimisha siku ya  mto Mara September 15 kila mwaka kwa kupokezana. ikiwa ni sehemu ya kuendeleza  juhudi za uhifadhi endelevu katika bonde la mto  huo .
Sherehe hizo zilifanyika Bomet  nchini Kenya mwaka jana .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages