TAZAMA VIDEO
Na Mwandishi wetu,
Kiongozi Mwenza wa
Chama Cha Wachungaji kutoka Makao Makuu ya kanisa la Waadventista Wasatabo(SDA) Ulimwenguni yaliyopo
Washington Marekani Pastor Anthony Kent yupo
Tarime katika kanisa la Sabasaba SDA kama mgeni maalumu katika semina ya
wachungaji , wazee wa kanisa na mashemasi wa kanisa hilo kutoka jimbo Mara ambayo imeanza leo
asubuhi.
Vijana wa pathfinder wakiwa katika sehemu ya mapokezi ya wageni |
Mchungaji Kent amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata na kueleza kuwa anajisikia yupo nyumbani huku akilifananisha kanisa la Sabasaba Tarime
kama bustani ya edeni.
Pr Anthony Kent akiwasalimia vijana wa pathfnder kwa mapokezi mazuri waliyompa, Kuhsoto ni Pr Enock Sando ambaye ni katibu wa Mara Confrence |
Akifungua mkutano huo Askofu wa Jimbo Kuu la
Waadventista Wasabato(SDA) Kaskazini mwa Tanzania Dkt Godwin Lekundayo amesema kazi kubwa ya
wazee wa kanisa ni kuwatunza
washiriki na sio tu kutoa matangazo
kanisani.
Dr Lekundayo amesema watu wengi wanaobatizwa katika
kanisa hilo wanapotea kwa sababu ya kukosa
mahusiano mazuri waliyoyategemea kuyapata kutoka kwa viongozi wa kanisa.
ijana wa pathfinder wakimsikiliza Pr Kent |
Katibu wa chama cha wachungaji jimbo la Mara
Mchungaji Joseph Matongo amesema wajumbe wa mkutano huo ni wachungaji na wake
zao, wazee wa kanisa, mashemasi na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo kutoka
ndani nan je ya nchi .
Congratulations!Keep it up to support the community in information technology!God uplift you more in the name of Jesus!
ReplyDelete