Wadau wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika Halmashauri ya Mji wa Tarime wamekutana leo Septemba 23, 2019 kujadili taratibu na kanuni za uchaguzi utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Jane Tungu amesema kuwa uchaguzi utafanyika kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni katika majengo ya umma na mitaa isiyo na majengo ya umma watapendekeza sehemu ambayo itakuwa rafiki kwa uchaguzi huo.
Miongoni mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa wadau uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Tarime ni uraia ,umri,utimamu wa akili na kutokuwa na kumbukumbu za uhalifu.
No comments:
Post a Comment